CONNEXION
  • RetourJeux
    • Sorties
    • Hit Parade
    • Les + populaires
    • Les + attendus
    • Soluces
    • Tous les Jeux
    • Gaming
  • RetourActu Gaming
    • News
    • Astuces
    • Tests
    • Previews
    • Toute l'actu gaming
  • RetourBons plans
    • Bons plans
    • Bons plans Smartphone
    • Bons plans Hardware
    • Bons plans Image et Son
    • Bons plans Amazon
    • Bons plans Cdiscount
    • Bons plans Decathlon
    • Bons plans Fnac
    • Tous les Bons plans
  • RetourJVTech
    • Actus High-Tech
    • Intelligence Artificielle
    • Smartphones
    • Mobilité urbaine
    • Hardware
    • Image et son
    • Tutoriels
    • Tests produits High-Tech
    • Guides d'achat High-Tech
    • JVTech
  • RetourCulture
    • Actus Culture
    • Culture
  • RetourVidéos
    • A la une
    • Gaming Live
    • Vidéos Tests
    • Vidéos Previews
    • Gameplay
    • Trailers
    • Chroniques
    • Replay Web TV
    • Toutes les vidéos
  • RetourForums
    • Hardware PC
    • PS5
    • Switch 2
    • Xbox Series
    • Switch
    • Pokemon pocket
    • FC 25 Ultimate Team
    • League of Legends
    • Tous les Forums
  • PC
  • PS5
  • Xbox Series
  • Switch 2
  • PS4
  • One
  • Switch
  • iOS
  • Android
  • MMO
  • RPG
  • FPS
En ce moment Genshin Impact Valhalla Breath of the wild Animal Crossing GTA 5 Red dead 2
Forum
  • Accueil
  • Actus
  • Tests
  • Vidéos
  • Images
  • Soluces
  • Forum
Liste des sujets

djibril cisse

toma_11
toma_11
Niveau 1
13 novembre 2005 à 19:45:57

donner tous une note a djib en equipe de france je ferai la moyenne
moi je donne 18/20
:merci:

clintyswood
clintyswood
Niveau 10
13 novembre 2005 à 19:46:37

Et moi je te donne 19,5/20 a ton topic inutile

coluche16
coluche16
Niveau 10
13 novembre 2005 à 19:47:06

Majaribio ya Chanjo ya Ukimwi kuanza nchini mwaka huu

2005-10-08 07:54:03
Na Haji Mbaruku

Wakati watalamu wa tiba za magonjwa sugu ukiwemo ukimwi wanaendelea na utafiti wa aina mbalimbali ili kupata chanjo na tiba ya ukimwi,hapa nchini baadaye mwaka huu inatarajiwa majaribio ya kwanza ya chanjo ya ukimwi kuanza kufanyika.

Majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI, iliyotengenezwa nchini Sweden kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya Muhimbili, yatarajiwa kuanza kutumika nchini kabla ya mwishoni mwa mwaka huu katika mkoa wa Dar es salaam.

Hata hivyo, majaribio ya chanjo hiyo nchini yatategemea matokeo ya majaribio ya dawa hiyo nchini Sweden, ambayo yalifanyika mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu kwa watu 40 wenye afya njema kuchanjwa.

Kwa mujibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi, Tanzania hadi kufikia mwaka 2003, ilikuwa na watu milioni 1.8 wanaoishi na virusi vya UKIMWI ( NACP).

Wizara ya Afya inasema kuwa, baada ya matokeo ya chanjo hiyo nchini Sweden kuwa salama na kupata mafanikio, chanjo hiyo itaendelezwa katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya cha Muhimbili, kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Karolinska cha Sweden pamoja na Taasisi ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza ya Sweden.

Utafiti uliofanywa na Mpango wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI, NACP na kuchapishwa kwenye jarida la Habari za UKIMWI linalotolewa na Wizara ya Afya unaonyesha kuwa, Taasisi zinazoshirikiana na Tanzania katika mkakati wa kutengeneza chanjo hiyo ni pamoja taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu ya Jeshi la umoja wa nchi za Amerika cha Walter Reed Army Institute, Chuo Kikuu cha Munich cha Ujerumani na Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini.

Pia, mipango ya kutengeneza chanjo ya UKIMWI inaendelea katika hospitali ya rufaa mkoani Mbeya.

Wizara ya Afya inasema kuwa, Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeathirika kwa kiwango kikubwa na ugonjwa hatari wa UKIMWI.Kutokana na kiwango kikubwa cha maambukizi ya virusi vya UKIMWI, chanjo ni muhimu kwa sababu itakuwa na uwezo wa kinga ya manufaa na ya kuaminika kwa watu wote watakaoshiriki.

Aina mbalimbali za virusi vya UKIMWI vinavyopatikana nchini ni tofauti na nchi nyingine, hivyo kuongeza umuhimu wa kufanya majaribio ya chanjo katika sehemu mbalimbali za nchi kunakopatikana aina tofauti ya virusi.

Kuanza kwa chanjo nchini kutatekelezwa chini ya mkakati wa chanjo ya UKIMWI wa Jamhuri ya Muungano nchini uliotengenezwa kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani, WHO na Mpango wa Umoja wa Mataifa wa UKIMWI, UNAIDS pamoja na programu ya dawa ya chanjo ya UKIMWI katika Afrika, AAVP.

Lengo kuu la mkakati huu ni kutoa mwongozo kwa sekta mbalimbali za serikali, taasisi na kwa wanasayansi nchini, ambao wanafanya utafiti pamoja na wadau wengine wa Taifa na kimataifa.

Wengine ni Jumuiya za wananchi na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuendeleza utafiti wa utengenezaji na kujaribia aina mbalimbali za chanjo dhidi ya virusi vya UKIMWI.

Tangu jaribio la awali kabisa la chanjo ya UKIMWI kwa binadamu mwaka 1987, zaidi ya aina 30 za chanjo zimekwishafanyiwa majaribio kwa binadamu.

Majaribio hayo yako katika hatua za mwanzo katika kupima usalama kwa binadamu na kupima uwezo wa kujenga kinga mwilini.

Hata hivyo, ni aina mbili tu za chanjo iitwayo VAXGEN ndizo zilizofanyiwa majaribio katika hatua ya tatu dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI nchini Marekani na Thailand.

Ingawa chanjo hizo zote zimeonekana kuwa salama kwa binadamu, hakuna iliyoweza kutoa kinga kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Wakati Taifa linaendelea na mikakati ya chanjo dhidi ya virusi vya UKIMWI, mikakati iliyopo wakati huu nchini itabidi iendelezwe. Mikakati ni pamoja na utoaji wa elimu ya kinga na kuongeza mwamko wa kutambua ugonjwa wa UKIMWI ili watu waweze kubadili tabia.

Mikakati mingine ni ushauri nasaha na upimaji wa hiari wa virusi vya UKIMWI ili wananchi waweze kujua iwapo wameambukizwa au la na kujua jinsi ya kuishi na kuzuia maambukizi mapya.

Iwapo majaribio ya chanjo yanayotarajiwa yatafanikiwa, zoezi la kuwachanja wananchi wote nchini litaanza kwa utaratibu utakaoandaliwa na wadau pamoja na wahusika wote.

Utafiti huo unaonyesha pia kuwa, idadi ya watu wanaojitokeza kupima Afya zao kwa hiari nchini imeongezeka, jambo linaloashiria kuwa uelewa kuhusu virusi vya UKIMWI na UKIMWI umeongezeka pia.

Kulingana na jarida hilo, Utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa jumla ya watu 139,972 walijitokeza kupima afya zao mwaka 2003, ikilinganishwa na watu 47, 956 waliojitokeza mwaka uliotangulia wa 2002.

Wizara ya Afya inasema kuwa ongezeko hilo ambalo ni mara tatu ikilinganishwa na mwaka uliotangulia, linatokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa hamasa miongoni mwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia huduma za ushauri nasaha na upimaji wa hiari.

Pia, watu wengi hivi sasa wanapata taarifa kuhusu mpango wa taifa wa huduma na tiba ambao hivi karibuni umeanza kutoa dawa kupunguza makali ya UKIMWI.

Sababu nyingine iliyosababisha kuongezeka kwa idadi ya watu wanaojitokeza kupata ushauri na kupima ni kuongezeka kwa idadi ya vituo vua ushauri nasaha na upimaji.

Idadi ya vituo hivyo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka kutoka vituo 59 mwaka 1997 hadi zaidi ya vituo 289 mwaka 2003.

Vituo 255 miongoni mwa hivyo, viko katika hospitali za serikali na zile za asasi za kidini, wakati 34 ni vya Angaza ambavyo viko chini ya shirika la Afya na Utafiti wa Tiba barani Afrika, AMREF.

Wizara hiyo inasema katika taarifa yake kuwa, jambo la kutia moyo katika utafiti huo, ambao umefanyika mwaka jana ni kuwa, ingawa idadi ya watu waliojitokeza kupima imeongezeka mara tatu, idadi ya watu waliopima na kukutwa na virusi imeonekana kupungua.

Kwa mfano, waliojitokeza na kupima katika vituo mbalimbali nchini kati ya mwaka 1997 na mwaka 2001, asilimia kati ya 59.5 na 76.0 ya watu walikutwa na virusi vya UKIMWI.

Hata hivyo, idadi ya waliojitokeza na kuonekana wameambukizwa, ilishuka hadi kufikia kati ya asilimia 18.9 mwaka 2002 na asilimia 18.4 mwaka 2003.

Takwimu hizo ni uthibitisho kuwa pamoja na sababu nyingine, idadi ya watu wanaokwenda kupima kwa hiari kwa lengo la kujua tu afya na kuwa makini zaidi ya kulinda afya yake kulingana na majibu atakayopata.

Mtu anapopima na kugundulika kuwa, ameambukizwa virusi vya UKIMWI, inamsaidia kujijua na kufuata taratibu na tahadhari mbalimbali ili yeye mwenyewe asiambukizwe na wala asiambukize wengine.

Aidha, wale wanaopima na kukutwa bado hawajaambukizwa virusi vya UKIMWI ambavyo baadhi vyaweza kuwa sugu kutokana na dawa zinazotumika za kupunguza makali, ARV,s.

Takwimu zinaonyesha kuwa, maelfu ya watu nchini wamekwishafariki kutokana na ugonjwa huo tangu ulipojitokeza zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Hivi sasa inakadiriwa kuwa , kati ya watu 400,000 na 500,000, wanahitaji dawa za kupunguza makali ya UKIMWI miongoni wa wanaokadiriwa kufikia milioni mbili wanaougua ugonjwa huo.Dawa za kupunguza makali ya UKIMWI, hupunguza kasi ya kuzaliana kwa virusi vya UKIMWI na hivyo kupunguza makali ya ugonjwa huo.

Vile vile, husaidia kuongeza kinga ya mwili na kuboresha afya ya mgonjwa, utoaji na usambazaji wa dawa hizo kwa sasa ni muhimu miongoni mwa mikakati ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI nchini.

Mkakati wa Taifa wa huduma za utoaji na usambazaji wa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI, ulipitishwa na Baraza la mawaziri mnamo Oktoba 2003 na mkakati wa mwaka wa kwanza umeshakamilika.

Kwa mujibu wa mkakati, hadi kufikia mwishoni mwa Mei 2005, hospitali zote 96 zimeanza kutoa dawa.

clintyswood
clintyswood
Niveau 10
13 novembre 2005 à 19:47:08

Non je rigole le prend pas mal :-)))

La vidéo du moment